Jumanne 1 Julai 2025 - 00:21
Makazi ya Imam Mahdi (as) katika Kipindi cha Ghaiba Kubwa

Hawza/ Ikiwa katika mada ya "ghaiba", mambo kama mahali alipo Imam (as), chakula chake n.k. yasibainike wazi, hilo halileti shaka wala dhana yoyote; vivyo hivyo, kubainika kwa mambo hayo hakuhusiki na uthibitishaji wa asili ya ghaiba.

Shirika la Habari la Hawza - Katika kipindi cha ghaiba kubwa, Imam Mahdi (as) anaishi wapi? Kimsingi, inapaswa kueleweka kuwa ikiwa katika suala la ghaiba, vipengele kama hivi vitabaki kutojulikana, hilo halisababishi shaka wala mashaka yoyote; kama ambavyo kubainika kwake hakuhusiki na kuthibitisha au kukanusha asili ya ghaiba. Na pale ambapo ghaiba ya Imam mwenyewe (as) na kujificha kwake ni jambo lenye mantiki na linalokubalika kiakili – kama ambavyo ni hivyo na tunaamini hivyo – basi kufichika kwa sifa hizi pia ni la kwanza kwa upande wa mantiki na akili, na kutojua mambo haya hakumaanishi chochote.

Pamoja na hayo, ili kutoa jibu jepesi kwa swali hili, tunasema kwamba kulingana na baadhi ya hadithi na masimulizi sahihi, Imam (as) katika ghaiba kubwa hana makazi ya kudumu mahali maalumu au katika mji maalumu kiasi kwamba asiutoke mji huo au kuhama sehemu nyingine. Bali huhama-hama kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake na kwa sababu ya kazi na wajibu wake, husafiri na kuzunguka kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Kulingana na baadhi ya masimulizi, ameonekana katika maeneo tofauti. Miongoni mwa miji ambayo bila shaka imebarikiwa na ujio wake ni: Madinah al-Tayyibah, Makkah tukufu, Najaf al-Ashraf, Kufah, Karbala, Kazimayn, Samarra, Mashhad, Qum, na Baghdad. Pia kuna maeneo na sehemu mbalimbali ambapo Yeye (as) ameshuhudiwa kuwa amekuwepo, kama vile: Msikiti wa Jamkaran mjini Qum, Msikiti wa Kufah, Msikiti wa Sahla, Maqam wa Sahib al-Amr katika Wadi al-Salaam ya Najaf na mjini Hilla.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba, makazi makuu au mahali ambapo huwepo zaidi ni Makkah tukufu, Madinah al-Tayyibah na maeneo matakatifu ya Atabat.

Iwapo mtu atauliza: Basi vipi kuhusu “Jabal Radwa” na “Dhi Tuwa” ambazo zimekuja katika "du‘ā’ al-Nudbah":

«لَیْتَ شِعْری أَیْنَ اسْتَقَرَّتْ بِکَ النَّوَی، بَلْ أَیُّ أَرْضٍ تُقِلُّکَ أَوْ ثَرَی أَبِرَضْوَی أَوْ غَیْرِهَا أَمْ ذِی طُوَی.»

“Laiti ningejua ni wapi moyo wangu ungepata utulivu kwa kuonekana kwako. Je, unakaa katika ardhi gani? Je, katika ardhi ya Radwa au mahali pengine, au katika Dhi Tuwa?”

Basi tunajibu kuwa: Sehemu hizi mbili – kwa mujibu wa vitabu vya lugha na historia – ni maeneo matakatifu, na kuna uwezekano kuwa Imam (as) hutumia sehemu hizi kwa ibada na kujitenga kwa ajili ya unyenyekevu. Hii haimaanishi kuwa maeneo hayo mawili au mojawapo ni makazi ya kudumu ya Imam (as).

Maswali kama haya hayamaanishi kuuliza kwa lengo la kupata jibu la kweli, bali ni maneno yanayotoka moyoni kutokana na uchungu wa kutengana, na majuto ya kutokumuona Imam na kuchelewa kwa kudhihiri kwake. Zaidi ya hayo, baadhi ya sentensi za "du‘ā’ al-Nudbah" zinabainisha kuwa Yeye (as) yupo miongoni mwa watu na si kwamba ametoweka kutoka kwao, kama ilivyosemwa:

«بِنَفْسِی أَنْتَ مِنْ مُغَیَّبٍ لَمْ یَخْلُ مِنَّا بِنَفْسِی أَنْتَ مِنْ نَازِحٍ لَمْ یَنْزَحْ (مَا نَزَحَ) عَنَّا.»

“Najiwekea fidiya nafsi yangu kwa ajili yako, ewe aliyeghaibishwa lakini hujatutoka! Najiwekea fidiya nafsi yangu kwa ajili yako, ewe uliye mbali lakini hujatutengana nasi!”

Iwapo mtu atauliza: Vipi kuhusu kauli ambayo husikika midomoni mwa baadhi ya watu, hasa baadhi ya wanazuoni wa Ahl al-Sunnah, na huwa wanaitumia kama kisingizio cha kuwashambulia na kuwatukana Shia – kwamba Mashia wanaamini kuwa Imam Sahib al-Amr (as) amejificha katika sardabu ya Samarra – hiyo inatokana na nini?

Jibu ni kwamba: Hili ni jambo lisilo na ukweli wowote, bali ni uzushi na tuhuma ya wazi, kauli hii haina msingi wowote wa kihistoria au wa kielimu.

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu “Majibu kwa Maswali Kumi Kuhusu Uimamu” kilichoandikwa na Ayatollah Safi Golpaygani – huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha